MKATE WA MCHELE/SINIA/KUMIMINA
Mahitaji:-
🔸Mchele vikombe 2 (vip ni mzuri zaidi kwa mikate na vitumbua)
🔸Hamira kijiko 1 1/2 cha chai
🔸Tui la nazi zito kikombe 1 1/2
🔸Sukari kikombe 1
🔸Hiriki ilopondwa kiasi
🔸Ute wa yai 1 (ukipenda)
NAMNA YA KUPIKA:
Hatua ya 1:
1. Loweka mchele katika maji kwa masaa kadhaa au usiku mzima upate kulainika
Hatua ya 2:
2. Chuja maji yote kisha utie katika blender pamoja na tui na hiriki kisha saga hadi mchanganyiko usagike ukibaki chenga chenga kidogo hakuna tabu zisiwe nyingi
Hatua ya 3:
3. Tia hamira na sukari kisha saga tena kuchanganya.Mimina katika bakuli,funikia acha sehemu yenye joto ufure hadi ujae mara mbili.
Hatua ya 4:
4. Ukiumuka tia ute wa yai, pia weza ongeza sukari kama imepelea kisha koroga vizuri kuchanganya.
Hatua ya 5:
5. Washa oven joto 180°C. Tia sufuria jikoni juu ya moto wa kiasi yakipata mimina mchanganyiko uache kwa muda wa dk 1 kisha tia kwa oven na oka kwa muda wa dk 30-35 au hadi upate rangi juu na kuiva.
Hatua ya 6:
6. Acha mkate upoe kabisa katika chombo chake hadi upoe kabisa. Enjoy!
unaweza oka kwa mkaa pia ukapalia.