FAIDA YA MATUNDA YA MZAITUNI
Habarini za leo wasomaji wetu. Natumai muko wazima wa afya.Leo nitawaelekeza matumizi sahihi ya Mafuta ya Zaituni (Olive Oil). Pia tutaona faida zinazopatikana kutokana na mafuta haya.
ZIFUATAZO NI BAADHI YA FAIDA ZA MAFUTA HAYA:
(1)Hutibu maumivu ya tumbo kwa kunywa kijiko 1 mara 2 kwa sikukwa muda wa siku 7 hadi siku 11 inshaallah utapona kabisa
(2)Mafuta ya zaituni hutibu masheitani kwa kusomea kisomo cha Ruqia, mgonjwa atajipaka mwili mzima mara moja kwa siku pamoja na kutafuna vitunguu saumu punje tatu wakati wa kulala kwa muda wa siku arobaini inshaAllah.
MWANAMKE INAKUHUSU FUNGUA HAPA. ☜
(3)Pia kinga ya masheitani wa kijini na wa kibinadamu kwa kujipaka mwili mzima mara moja kwa siku.
(4)Hutibu ugonjwa wa mafua kwa kupaka kwenye mwamba wa pua na ndani ya matundu ya pua mara tatu kwa siku.
(5)Tiba ya vidonda vya tumbo; Matumizi ni kutia vijiko 2 vya chakula katika uji mara mbili kwa siku kwa muda wa siku 90.
(6) Mafuta ya zaituni hutumika kama huduma ya kwanza kwa aliyekunywa sumu kwa kunywa, na kwa mwenye ganzi au kiharusi hutumia kwa kuchua mwilini asubuhi na jioni.
FAIDA NA TIBA ZA MAFUTA YA MZAITUNI
(7) Mafuta ya zaituni hutumika katika kuua wadudu wabaya walioko tumboni kwanjia ya kunywa kijiko kimoja mara mbili kwa siku kwa muda wa siku saba.
(8) Mafuta ya zaituni huongeza nguvu za kiume kwa kunywa kijiko kimoja kwa siku pamoja na kuuchua uume mafuta yaliyochanganywa na vitunguu swaumu kwa muda wa siku saba hadi kumi na moja.
(9) Tiba ya ugonjwa wa kusahau: paka katika paji la uso kutwa marambili pamojana kunywa kijiko kimoja cha chai mara moja kwa siku kwa muda wa siku 7 hadi siku 11.
OPEN THIS
(10) Tiba ya degedege: hutumika kupakaa mwili mzima mafuta yaliosomewa ruqya, marambili kwa siku kwa muda wa siku 7 hadi siku 21.
(11)Kukojoa kitandani: kupakaa mafuta ya zaitun mwili mzima kutwa marambili huku akilamba matone mawili kwa muda wa siku 7 hadi siku 21.
BAADHI YA FAIDA ZENGINE NI KAMA VILE
(12) Husaidia kupunguza mafuta mwilini.Mafuta haya yanajulikana kama kolestero (Cholesterol).
KWA AJILI YA AFYA YAKO SOMA HAPA. ☜
(13) Inapunguza makali ya njaa.
(14) Utumiaji wa mafuta haya unapunguza hatari ya ugonjwa wa moyo (coronary heart disease) hasa kwa wanawake.
(15) Yanasaidia kuzuia kansa ya matiti. Mafuta haya yana phytochemicals ambayo inasaidia kuzuia kansa.
Kwa kweli faida za haya mafuta ni nyingi sana. Unaweza soma faida zake zaidi kupitia hii : https://www.robbinsfamilyfarm.com/101-olive-oil-benefits/