JINSI YA KUTENGENEZA PEANUT BUTTER - SIAGI YA KARANGA

 JINSI YA KUTENGENEZA PEANUT BUTTER - SIAGI YA KARANGA


♦MAHITAJI

👉 Karanga vikombe 2

👉 Asali au sukari kijiko 1 na nusu cha chakula

👉 Mafuta ya kupikia kijiko 1 na nusu cha chakula

👉 Chumvi ½ kijiko cha chai



♦NAMNA YA KUTAYARISHA

1.Kaanga karanga bila mafuta mpaka zikaangike vizuri yani maganda yaanze kutoka yenyewe

2.Ziache zipoe kisha toa maganda

3.Mimina karanga,chumvi na mafuta katika blender ama food processor...saga hadi iwe laini

4.Ongeza asali,chumvi ,sukari au asali na mafuta saga hadi iwe laini...

5.Hifadhi katika chupa yako kisha weka kwenye FriJi

NB ; UKILA NA MKATE USISHANGAE KUSIKIA KITU KINAKUAMBIA UKANUNUE MKATE MWINGINE MZIMA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad