Kutokwa na harufu mbaya ukeni ni tatizo linalowasumbua wanawake wengi duniani, hususani wakati wa tendo la ndoa. Kutokwa na harufu mbaya ukeni kwa kiasi kikubwa husababishwa na fangasi wa candida, japo sio kila mara ndio maana kuna umuhimu wa kutafuta chanzo cha tatizo la kunuka uke.
Kutoa harufu mbaya ukeni huweza kuambatana na dalili zingine kama vile; Miwasho sehemu za siri, hisia za kuungua sehemu za siri, michomo na kutokwa uchafu sehemu za siri.
Sababu Za Uke Kutoa Harufu Mbaya:
Zipo sababu nyingi zinazopelekea mwanamke kutokwa na harufu mbaya ukeni, baadhi ya sababu hizo ni pamoja na;
A) Magonjwa Ya Zinaa (Sexually Transmitted Diseases).
Mfano wa magonjwa ya zinaa ni pamoja na kisonono, kaswende, Trichomoniasis n.k. Magonjwa haya yasipotibiwa kwa wakati hupelekea mwanamke kutoa harufu mbaya ukeni.
B) Matumizi Mabaya Ya Dawa Za “Antibiotics”.
Hutumiaji kiholela wa dawa hizi bila ushauri au maelekezo ya wataaalamu wa afya (daktari) ni mojawapo ya sababu ya mwanamke kutoa harufu mbaya ukeni. Hivyo ni vyema mwanamke akafuata ushauri na maelekezo ya wataalamu wa afya kabla ya kutumia dawa za Antibiotics.
C) Kutozingatia Usafi Na Kutokwa Sana Na Jasho.
Ni wazi kwamba uchafu na kuwepo kwa unyevunyevu sehemu za siri huzalisha harufu mbaya.Kisayansi ni kwamba tezi zilizopo ndani ya mwili (Apocrine sweat glands) hutengeneza mafuta kuelekea kwenye maeneo ya mwili.
D) Maambukizi Katika Via Vya Uzazi (Pelvic Inflammatory Disease).
Pelvic Inflammatory Disease (PID) hili ni tatizo linalotokana na magonjwa sugu ya zinaa kama vile gonorrhea, chlamydia. Hivyo magonjwa ya zinaa ambayo hayakugundulika mapema, tiba hafifu, au uzembe wa kutumia dawa ni chanzo kimojawapo cha mwanamke kutoa harufu mbaya ukeni.
E) Bacterial Vaginosis.
Kwa kawaida mwili wa binadamu una bakteria wa aina mbili, bakteria rafiki (normal flora) na bakteria adui (pathogens) ambapo ukeni kuna bakteria rafiki kwa kiwango kinachohitajika, bakteria hawa wanapoongezeka na kuvuka mahitaji huwa sio rafiki tena, huanza kushambulia sehemu ya uke na kuruhusu maambukizi ambayo hutoa majimaji yenye harufu mbaya ukeni.
F) Mabadiliko Ya Homoni.
Mabadiliko ya homoni kutokana na mzunguko wa hedhi unaweza kuchangia harufu mbaya ukeni. Wanawake wanaokaribia kukoma hedhi (menopause) wapo kwenye hatari zaidi kwani homoni ya estrogen hupungua sana na hivo kusababisha tishu za kuwa na tindikali kidogo.
Dawa Za Kutibu Harufu Mbaya Ukeni:
Kutoa harufu mbaya kwenye uke mara nyingi inagundulika zaidi baada ya kufanya ngono na pia kwenye hedhi. Kwa hiyo badala ya kukimbilia spray na kujisafisha ukeni ili kuondoa harufu tumia njia zifuatazo kwa muda kabla hujamuona daktari wako;
1) Apple Cinder Vinegar:
Vinegar hii imejaa viini ambavyo ni anti bacterial na antispetic ambavyo vitakusaidia kupambana na harufu mbaya ukeni.
Jinsi Ya Kutumia Apple Cinder Vinegar Kuondoa Harufu Mbaya Ukeni:
Chukua kiasi kidogo cha Vinegar changanya na maji kwa uwiano wa 1/10 na uoshe eneo la uke.
2) Baking Soda:
Baking soda inaweza kutumika ili kubalansi pH kwenye mwili. Ukibalansi pH basi tatizo la harufu mbaya ukeni linakuwa limeisha. Unaweza kutumia pia baking soda kama body spray na kuepuka kujaza sumu mwilini.
Jinsi Ya Kutumia Baking Soda Kuondoa Harufu Mbaya Ukeni:
Chukua kijiko kimoja cha baking soda weka kwenye ndoo na maji jagi moja, kisha osha uke kwa dakika 5, Jifute kwa taulo sehemu zote usiache unyevu kabla ya kuvaa nguo.Tumia mara mbili tu kwa wiki usizidishe.
3) Kitunguu Saumu.
Kitunguu saumu kinafahamika tangu miaka ya zamani kwa uwezo wake mkubwa wa kuimarisha kinga ya mwili na kupambana na maambukizi ya bakteria na fangasi.
Jinsi Ya Kutumia Kitunguu Saumu Kuondoa Harufu Mbaya Ukeni:
Unaweza kula kitunguu saumu kimoja kwa siku ama ukatumia virutubisho ambavyo vipo kwenye mfumo wa vidonge mfano Garlic ambavyo tunatumia kuwahudumia wagonjwa wetu.
4) Matunda Na Mboga Mboga.
Matunda yenye uchachu mfano machungwa, mapera na straw berries yana vitamini c kwa wingi sana ambayo huimarisha kinga ya mwili na husaidia utoaji wa sumu wilini. Chakula kama parachichi na mbogamboga za kijani zina viamini B6 na madini ya potassium ambayo huongeza hamu ya tendo la ndoa na kujenga kuta za uke hivyo kuzuia hatari ya kushambuliwa mara kwa mara.
5) Karanga Na Mbegu.
Matumizi ya karanga na mbegu kwenye mlo wako wa kila siku huzuia kukauka kwa uke kwa sababu kwenye karanga kuna vitamini E kwa wingi. Unaweza kutafuna mbegu za maboga, almond, karanga, walnuts na alizeti.
6) Maji Safi Ya Kunywa.
Kiungo hiki cha uke chenye tishu laini kinahitaji maji ya kutosha ili kukiweka laini na hivyo hupunguza harufu mbaya ukeni. Unashauriwa unapopata kiu usinywe soda, kunywa maji ya kutosha.
7) Sabuni Ya Kuondoa Harufu Mbaya Ukeni.
Unashauriwa kutumia sabuni ya maji iitwayo care isiyokuwa na kemikali yoyoye hatarishi kwenye uke. Tumia sabuni hii kusafisha sehemu ya nje ya uke tu na kufulia nguo za ndani (chupi). Sabuni hii husaidia pia kumaliza kabisa miwasho sugu, mapunye, mba na harara, humaliza kabisa fangasi sugu sehemu za siri
Jinsi Ya Kutumia Sabuni Ya Maji (Care) Kuondoa Harufu Mbaya Ukeni:
Chukua kiasi kidogo cha sabuni ya maji (care) kisha changanya kwenye maji yako ili kutengeneza povu, baada ya hapo tumia maji hayo yenye sabuni ya care kujitawazia sehemu za siri, kufulia na kusuuzia nguo zako za ndani (chupi).
Tahadhari: Mama mjamzito haruhusiwi kutumia sabuni ya maji (care).
Jinsi Ya Kusafisha Uke Baada Ya Tendo La Ndoa:
Sehemu za siri za Mwanamke zimegawanyika katika sehemu kuu mbili.
Kuna sehemu ya nje (Outer part) na kuna Sehemu ya ndani (Inner part).
Hivo basi hata katika kusafisha uke wako unatakiwa kuzingatia kwa makini maeneo haya. Sehemu ya ndani pamoja na sehemu ya nje. Sehemu ya ndani ya Uke hairuhusiwi kuoshwa au kuguswa na kitu chochote kama sabuni nk.
Kwani sehemu hii hujisafisha yenyewe (self cleansing) na kutoa uchafu nje, hivyo sehemu ya kuosha ni sehemu ya nje ya uke tena kwa uangalifu mkubwa.
Kumbuka:
Mambo Ambayo Mwanamke Hatakiwi Kufanya Wakati Wa Kusafisha Uke Wake:
Yafuatayo ni mambo ambayo mwanamke ashauriwi kufanya hasa wakati wa kusafisha uke wake;
1) Vaginal Douching.
Hii ni ile tabia ya kuosha sehemu nza ndani ya uke kwa kutumia viosheo maalumu vinavyopatikana madukani au super markets mbalimbali. Pia vaginal douching ni kule kutumia sabuni za maji au maji maalumu ambayo yanakuwa yamechanganywa na iodine, vinegar, magadi na kuyaingiza ndani ya uke, hii ni hatari kwa afya ya uke wako.
Ikumbukwe vaginal douching ni tofauti kabisa na ule unawaji wa kawaida au uoshaji wa kawaida wa uke wakati wa kuoga kwani haijakatazwa kuosha uke kwa maji ya uvuguvugu kwani ni salama na hakuna matatizo kiafya.
Njia bora ya kusafisha uke ni kutumia maji ya vuguvugu pale unapooga kwa kusafisha sehemu za nje na sio ndani ya uke kwani sehemu ya ndani uke hujisafisha wenyewe (vagina is self cleansing).
b) Vaginal steaming.
Hiki ni kitendo cha kujifukiza uke kwa kutumia marashi yaitwayo YONI STEAM ambapo mwanamke hukaa juu ya kiti ambacho chini yake kuna bakuli yenye maji ya moto na mvuke huo huenda moja kwa moja kwenye sehemu za uke. Kitendo hiki hufanywa kwa nia ya kusafisha uke lakini kimepigwa vita na madaktari wengi ambao wanaeleza kuwa kitendo hiki huwaondoa bakteria wanaotakiwa katika kurekebisha mfumo wa homoni na hivyo kusababisha madhara.
HITIMISHO:
Kwa wanawake wenye changamoto ya kupata muwasho kwenye uke, mnashauriwa kutumia virutubisho lishe vilivyotokana na mimea na matunda (Garlic) na sabuni ya maji (care) isiyo na kemikali yoyote hatarishi kwenye afya ya uke.