JINSI YA KUPIKA BOFLO MKATE WA ZANZIBAR.
MAHITAJI NA VIPIMO.
Kipimo cha mikate miwili
i. Unga mweupe - 6 vikombe (29 ounces takriban)
ii. Hamira - 2 vijiko vya chai
iii. Siagi (butter) - 2 Vijiko vya kulia
iv. Maji ya vuguvugu (warm water) - 1 kikombe
v. Maziwa vuguvugu (warm milk ) - 1 kikombe
vi. Sukari - 2 Vijiko vya kulia
vii. Chumvi - 1 kijiko cha chai
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA MKATE WA BOFLO.
1. Weka katika bakuli la mashine (electrical bowl) hamira, maziwa, sukari chumvi na siagi iliyoyaushwa. Changanya vizuri kwa mwiko.
2. Tia unga pole pole huku umeasha mashine ikande, ukiongezea unga mpaka umalizike.
3. Pakaza siagi bakuli jengine kubwa kisha mimina mchanganyiko. Funika kwa kitambaa kilichokuwa kimeloa maji (damp cloth) au karatasi ya plastiki (plastic wrap). Uache unga uumuke mpaka uwe saizi ya mara mbili yake.
4. Utoe hewa unga na umimine juu ya baraza (flat surface). Gawa mchanganyiko sehemu mbili umimine katika treya ya loaf (loaf pan) size ya treya 9 x 5 inchies takriban. Acha uumuke tena kiasi nusu saa.
5. Washa oveni mapema kiasi 200 Degrees uchome (bake) kaisi nusu saa mpaka ugeuke rangi ya hudhurungi (golden brown).
6. Epua upoe ukiwa tayari