- Unga wa ngano (self risen flour 2 vikombe vya chai)
- Sukari (sugar 1/2 kijiko cha chakula)
- Chumvi (salt 1/2 kijiko cha chai)
- Hamira (yeast 1/2 kijiko cha chakula)
- Baking powder 1/2 kijiko cha chai
- Siagi (butter 1/4 ya kikombe cha chai)
- Maziwa (fresh milk 3/4 ya kikombe cha chai)(unaweza kutumia maji badala ya maziwa)
Matayarisho
Pasha maziwa yawe ya uvuguvugu
kisha weka pembeni, pia yeyusha siagi na uweke pembeni.Baada ya hapo tia
kila kitu kwenye bakuli la kukandia kasoro maziwa, na uchanganye vizuri
kisha tia maziwa kidogo kidogo katika mchanganyiko huo kisha ukande.
Ukimaliza uweke kwenye sehemu ya joto na uache uumuke. Ukisha umuka
utawanyishe katika madonge saba Kisha .pakaza mafuta au siagi katika
chombo cha kuokea kisha yapange hayo madonge katika hicho chombo na
uyaache yaumuke tena (kwa mara ya pili). Baada ya hapo pakaza mafuta juu
ya hayo madonge na uyaoke (bake) katika oven (moto 200°C ) kwa muda wa dakika 25 na hapo scones zitakuwa tayari
ANGALIA VIDEO HII