MALIGHAFI
Vipimo
- Mchele - 3 vikombe vya chai
- Sukari - 2 kikombe cha chai
- Hamira - 1 kijiko cha chai
- Ute wa yai - 1 yai
- Tui la nazi - 4 kikombe cha chai
- Hiliki - kiasi
- Mafuta (ya kupakia treya) - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Roweka mchele kwenye maji usiku kucha.
- Chuja mchele kisha tia kwenye mashine ya kusagia (blender) usage pamoja na hamira, sukari, iliki na tui la nazi.
- Mimina ndani ya bakuli na ufinike. Weka mahali penye joto ili mchanganyiko uumuke(ufure).
- Kisha tia ute wa yai koroga vizuri .
- Paka mafuta kwenye treya au sufuria ya kuchomea kisha mimina mchanganyiko wa mchele .
- Choma (Bake) kwenye oveni kwa moto wa 350°C kwa dakika 30-45, kisha weka moto wa juu (grill) kama dakika 5-10 mpaka ubadike rangi kwa juu.
- Utoe kisha ukate vipande pande ukishapoa weka kwenye sahani tayari kwa kuliwa.
ANGALIA VIDEO HII