JINSI YA KUPIKA MANDAZI YALIYO NA LADHA YA APPLE

MAHITAJI
  • Unga wa ngano 250 g
  • Hamira kijiko 1
  • Mayai 2
  • Maziwa ½ kikombe
  • Apple 4
  • Chumvi ½ kijiko
  • Mafuta ya kula
JINSI YA KUANDAA
  1. Kwenye bakuli, weka unga na hamira kisha changanya vizuri. Pasua mayai, chuja kiini na ute. Weka viini kwenye unga pamoja na sukari kidogo. Changanya pamoja vizuri.
  2. Weka maziwa kwa awamu huku unaendelea kuchanganya unga. Dida likiwa na uzito ulio wastani weka ute wa yai, uwe umekorogwa vizuri.
  3. Menya apples, kisha kata kwenye vipande vya uviringo vya wastani vilivyo sawa. Chovya vipande kwenye dida vinyonye dida kwa juu.
  4. Bandika mafuta jikoni, acha yapate moto vizuri. Yakishapata moto weka vipande vya apple, acha viive kwa dakika 3 hadi 5. Kisha toa na weka pembeni kwenye chombo kisafi.
  5. Rudia hatua hii hadi vipande vyote vya apple na dida viishe.
  6. Unaweza kuweka sukari na coating tofauti za icing sugar kwenye haya maandazi ili kukupa ladha.
  7. Unaweza kula maandazi haya upendavyo – kwa chai, kawaha, maziwa, au kwa kulumagia. 
ANGALIA VIDEO HII

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad