JINSI YA KUPIKA CHAPATI ZA VIAZI

 JINSI YA KUPIKA CHAPATI ZA VIAZI


MAHITAJI

♦DONGE

👉 Unga wa ngano vikombe 4

👉 Mafuta viJiko 2 chakula

👉 Maji kiasi

👉 Siagi ½ kikombe

♦UPANDE WA VIAZI

👉 Viazi vilivyochemshwa na kupondwa 4

👉 Chumvi kiasi

👉 Binzari ya unga ½ kiJiko chai

👉 Pilipili ya unga ½ kiJiko chai/ukipenda

👉 Kitunguu kilichokatwa katwa 1



MATAYARISHO NA JINSI YA KUPIKA.

1. Changanya mahitaji yote ya unga kisha kanda kufanya unga mlaini.

2. Funika acha ukae ½ saa, fanya madonge size upendayo.

3. Changanya mahitaji yote ya viazi weka pembeni.

4. Chukua donge moja sukuma kufanya chapati ndogo, chota mchanganyiko wa viazi kisha funika vizur na zungusha kufanya donge tena. Rudia kwa madonge yote.

5. Sukuma chapati zako na choma kama kawaida katika moto wa kiasi hadi zipate rang nzuri.

6. Chapati za viazi tayari kwa kula na curry yoyote.

NB ; UKIWA UNASHUSHIA NA FANTA PEMBENI LAZIMA USAHAU SHIDA ZA DUNIA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad