Mahitaji
- Vipande vya kuku kilo 1
- Mchele wa basmati gramu 400 (unaweza kutumia mchele unaopenda)
- Kitunguu maji 1
- Nyanya zilokatwa 5
- Vitunguu saumu punje 5
- Pilipili za kijani 4
- Mafuta ya kula vijiko vya chakula 4
- Mdalasini vijiti 4
- Hiliki 3-4
- Tangawizi iliopondwa vijiko vya chakula 2
- Majani ya nanaa yaliyokatwa kiganja 1
- Binzari nyembamba kijiko cha chai 1
- Chumvi kijiko cha chai 1
- Manjano kijiko cha chai ½
- Zaafarani kijiko cha chai ½ (si lazima)
- Kotmiri iliyokatwa kikombe ¼
Matayarisho
Loweka mchele wa basmati kwenye maji na uweke pembeni kwa dakika 15 hadi 30 (kama hutumii mchele wa basmati basi utaangalia mwenyewe mchele unaotumia)
Maelekezo
- Weka mafuta kwenye sufuria, yakipata moto kaanga kitunguu maji hadi view na rangi ya kahawia.
- Twanga kwa pamoja binzari nyembamba, kitunguu swaumu, tangawizi, nusu ya pilipili na vijiti viwili vya mdalasini, kisha weka kwenye vitunguu ukaange pamoja kwa dakika tatu.
- Tia nyanya na pika kwa dakika tano
- Tia vipande vya kuku koroga, acha iwive kiasi cha dakika 10 hadi 15 na ikaukie
- Weka pilipili zilobaki kotmiri na masala ya kuku. Pika rosti liwe zito.
- Acha rosti na weka pembeni.
- Chemsha maji kwa hiliki na mdalasini na chumvi kisha weka mchele lakini usiwive kabisa kwa dakika tano baada ya hapo mwaga maji.
- Panga wali na masala.
- Kwanza chemsha maji ½ kikombe katika sufuria utakayopikia biryani. Maji yakishachemka anza kuweka wali kisha rosti na malizia na wali. Kama una tumia zaafarani…
- Zaafarani kawaida hurowekwa kwenye vijiko vyenye maziwa ya vugu vugu na kumwagilia kwa juu.
- Weka moto mdogo kwa dakika 30. Baada ya hapo chakula chako kitakuwa tayari.
JINSI YA KUPIKA BIRYANI LA KUKU.