Vipimo
Mayai yaliochemshwa - 6
Nyama ya kusaga - 1 1/2 Ratili (LB)
Tangawizi na Kitunguu saumu(thomu) iliyosagwa - 1 kijiko cha Supu
Pilipili mbichi ya Kusaga - 1
Mafuta - 2 Vijiko Vya Supu
Unga wa mahindi (Constarch) - 1 Kijiko cha Supu
Chumvi - Kiasi
Bizari ya manjano - 1/4 kijiko cha chai
Dania ya unga - 1/4 Kijiko cha chai
Bizari ya Pilau - 1/4 Kijiko cha chai
Namna ya kutayarisha na kupika
- Changanya nyama na vitu vyake kisha gawanya madonge 6 yaliyosawa.
- Chukuwa donge moja tia ndani yake yai uliochemsha na lifunike vizuri.
- Ukisha maliza yote panga kwenye treya la kupikia katika jiko la oveni nyunyizia mafuta kidogo na choma moto wa 375F kwa muda wa dakika 25.
- Yakishaiva epua na kisha ukate kama ilivyo kwenye picha .Tayari kuliwa .