Vipimo
Maharage - 3 Vikombe
Tui la nazi zito - 1½ kikombe
Kitunguu - 1 kikubwa
Nyanya - 2 au tatu
Kitunguu saumu (thomu/galic) iliyosagwa - 1 kijiko cha supu
Bizari ya mchuzi - 1 kijiko cha chai
Bizari ya manjano - robo kijiko
Pilipili mbichi - 3
Chumvi - Kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Roweka maharage, kisha chemsha maharage hadi yawive yabakie na supu yake kidogo
- Katakata kitunguu, nyanya, na thomu
- Kaanga kitunguu kidogo kisha tia thomu, nyanya, kisha kaanga,
- Tia bizari ya mchuzi na ya njano kaanga kidogo.
- Tia tui la nazi na acha kidogo tu katika moto.
- Weka chumvi kiasi na koroga iliuonje, kisha tupia pilipili mbichi, mimina katika chombo yakiwa tayari kuliwa