KUPIKA KABABU

Upishi wa Kebabu


Mahitaji
1. Nyama ya kusaga kl 1
2. Kotmili/giligilani wengine huita kifungu kimoja
3. Kitunguu maji vikubwa vitatu
4. Swaum kikubwa kimoja n tangawizi

5. Mikate ile ya buku miwili ama mitatu
6. Chumvi kiasi
7. Binzali nyembamba na pilipili manga vilivyo sagwa
8. Pili pili hoho kubwa moja
9. Mafuta ya kupikia
10. Ndimu
11. Mayai sita
Wapishi wenzangu Asalaam Aleykum kwa cc waislam n Bwana acfiwe kwa upande wa pili.
Haya jongeeni kijiweni tuongezeane ujuzi wa mapishi. Angalia upishi wa KEBABU.

 Kuandaa
Nyama ya kababu hua aichemshwi habisa. Kumbuka nyama kama ina maji kumbuka kuyakamua. Chukua nyama yako weka kwenye chombo kisafi, tia chumvi, ndimu, unga wa binzari nyembamba na pilipili manga, alafu changanya huo mchanganyiko wako na uwakikiche umechanganyika vizuri kabisa.

Hatua inayo fuata.
Katakata vitunguu maji katika vipande vidogo vidogo kama vya sambusa vile, oya kotmili/giligilani zako vizuri na ukamue maji alafu toa ile mizizi ya nyuma na kisha katakata katika vipande vidogo vidogo, twanga swaum zako na badala ya hapo tia katika mchanganyiko wako ule wa nyama. Changanya mpaka uakikiche umechanganyika vizuri. Kuonja ruksa wapenzi iliuweze jua kama vitu vuote vipo sawa au laa….
Hatua ya tatu.
Chukua mikate yako toa ile nyama ya kati nikimaanisha ile nyama ya mkate nyeupe ule upindo wa pembeni ucweke sababu ni mgumu na co soft. Chambua mikate yako vizuri kabisa na inyambue nyambue na uweke katika mchanganyiko wako wa nyama, chukua mayai matatu uweke humo. Changanya vyote sasa kwa pamoja mpaka uwakikiche vimechanganyika ipasavyo. Na baada ya hapo utafanya kama unakanda unga wa ngano vilee na upate donge moja takatifu. Utaacha mchanganyiko wako kwa mda wa kama dk 10 or 15 hivi ili viungo viweze kukolea kwa uzuri.
Hatua ya nne na mwisho.
Kata vidonge vidodo vidogo ama upendavyo na kutengeneza style uipendayo, weka kwenye chombo safi, vyunja mayainyako yale matatu yalio baki na uweke kwenye bakuli toa vile viini vya ndani na ubaki na ute tu. Weka flampeni/karai lako jikoni na ucwe na moto mkali, moto uwe wa wastani tu, mafuta yako yakisha pata moto chukua kebabu zako tosa kwenye ule ute wa yai na uweke kwenye mafuta yakio jikoni na utarudia kwa vyote viduara ulivyo fanya. Baada ya hapo vitakua tayari kwa kuliwa. 
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad