Kuandaa Biskuti Za Mtindi

Biskuti Za Mtindi/Yoghurt

Vipimo
  • Chenga za biskuti  -  3 gilasi
  • Mtindi (yogurt)  -  1 Kopo (750g)
  • Maziwa ya unga  -  1 gilasi
  • Siagi   -  10 Vijiko vya supu
  • Sukari -  ½ gilasi
  • Lozi zilizomenywa vipande vipande - ½ gilasi
  • Nazi iliyokunwa -  ½ gilasi
  • Vanilla  -    1 Kijiko cha supu


Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
  1. Katika mashine ya kusagia (blender), tia mtindi, sukari, siagi na vanilla na usage pamoja hadi ichanganyike.
  2. Mimina katika bakuli la kiasi.
  3. Tia vitu vilivyobakia na uchanganye vizuri.
  4. Mimina kwenye treya ya kuchomea na uvumbike katika oveni moto wa 350° hadi ishikamane na kuwa tayari.
  5. Iaache ipoe kisha katakata vipande na tayari kwa kuliwa.
Kidokezo:

Baada yakuwa imeshaiva, ukipenda unaweza kupakiza jamu au karameli ya tayari kwa juu, kisha ukarudisha kwenye oveni moto wa juu kidogo kwa ladha nzuri zaidi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad