KUTENGENEZA SAUCE YA TOMATO


Yafuatayo ndiyo mahitaji ya kutengeneza tomato source.

  1.  Nyanya kilo 1.
  2.  Vitunguu maji viwili.
  3.  Vinegar vijiko 3 vya chai.
  4. Sukari vijiko 2 vya chai.
  5. Chumvi kijiko kimoja cha chai
  6.  Maji ya moto kikombe kimoja cha chai.
  7.  Mafuta ya kula vijiko 7 ya vyakula.



Haya ndiyo mahitaji ya kutaka kutengeneza tomato souce, hata hivyo kama unataka kutengeneza zaidi ya hapo unatakiwa kuongeza uwiano wa mahitaji hayo.

JINSI YA KUTENGENEZA TOMATO SOURCE.


HATUA YA KWANZA.

a) Menya nyanya na vitunguu kisha vikate vipande vidogo vidogo.

b) Tumia Brenda kusaga mchanganyiko wako.

c) Anza kuweka malighafi namba 1 hadi namba 4 katika brenda yako kutokana na ratio (uwiano ) uliopewa hapo juu. Saga kwa dakika kadhaa hadi uone imetokea rojo laini.

HATUA YA PILI.
a) Tumia sufuria yenye nafasi kupika mseto huu.

b) Weka sufuria yako jikoni tia mafuta ya kula acha yachemke kisha mwagia mseto wako na kisha uanze kukoroga kwa dakika 30 kuelekea upande mmoja huku ukichemka.

c) Baada ya hapo epua mseto huo utakuwa tayari imeshakukua tayari kutumika
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad