Watu wengi hupenda kupaka mafuta ya zaituni (olive oil) hasa kuchua mwili (massage) au kwa kupikia kutokana na kuwa na manufaa mengi katika mwili wa binadamu.
Mafuta ya zaituni yanatokana na tunda liitwalo zaituni. Tunda hili ambalo lipo la kijani na jeusi, linaliwa kama ilivyo matunda mengine.
Mti wake unastawi na kuzaa vizuri ikiwa utapandwa kwenye sehemu zenye joto.
Matunda haya hupatikana zaidi nchi zenye jangwa hasa mashariki ya kati.
Magonjwa na tiba yake
Mafuta ya zaituni hutibu maumivu ya tumbo kwa kunywa kijiko kimoja mara mbili kwa siku, ndani ya wiki moja au zaidi.
Kwa wale wenye tatizo la kukojoa kitandani wanapaswa kupaka mafuta ya zaituni mwili mzima mara mbili kwa siku huku wakilamba matone mawili wakati wa kulala ndani ya wiki moja hadi tatu. Mafuta haya pia, ni tiba ya degedege na hutumika kupakaa mwili mzima mara mbili kwa siku 21.
Mafuta ya zaituni hutibu mafua kwa kupaka kwenye mwamba wa pua na ndani ya matundu ya pua mara tatu kwa siku.
Pia ni tiba ya vidonda vya tumbo; matumizi yake ni kutia vijiko viwili vya chakula katika uji mara mbili kwa siku 90.
Mafuta haya pia hutumika kama huduma ya kwanza kwa mtu aliyekunywa sumu kwa kunywa nusu kikombe cha mafuta hayo mara moja.
Kwa mwenye ganzi au kiharusi, wanapaswa wachanganye mafuta hayo na halmiti na irikizamda kisha wanywe kutwa mara tatu.
Pia, ni tiba ya ugonjwa wa kusahau; ukiwa na tatizo hilo paka mafuta haya katika paji la uso kutwa mara mbili pamoja na kunywa kijiko kimoja cha chai mara moja kwa siku, kwa zaidi ya wiki moja.
Pia, nywele hazitakatika hovyo wala kupukutika kwa kuwa mafuta hayo huua mba kichwani.
Kwa watu wanaokabiliwa na maumivu ya sikio kutokana na sababu mbalimbali, tiba yake ni mafuta ya zaituni.
Unachotakiwa kufanya ni kutwanga kitunguu saumu kisha changanya na mafuta ya zaituni, yapashe moto yawe vuguvugu. Hakikisha yasiwe ya moto kiasi cha kukuunguza.
Dondoshea matone mawili (muda wa kulala usiku), mara mbili kwa wiki. Ziba na pamba hadi asubuhi.
Mwandishi wa makala haya ni daktari wa tiba mbadala.