- Kitunguu maji 1
- Karoti 3
- Viazi ulaya robo kg
- Sweetcorn 50g
- Maziwa robo lita yaliyochemsha kabisa
- Kuku aliyechemshwa na asiye na ngozi wala mifupa robo kg
- Supu ya kuku kikombe 1
- Butter yenye chumvi 25g
JINSI YA KUANDAA
- .Washa moto, bandika sufuria jikoni.
- Weka butter ikiyeyuka na kuchemcha, weka kitunguu maji, koroga kwa dakika 1, weka karoti endelea kukoroga kwa dakika 5.
- Weka viazi na kuku ( mkate vipande vidogo sana) endelea kukoroga kwa muda, ongeza mchuzi.
- Funika vizuri mvuke usitoke, funika kwa dakika 15.
- Weka sweetcorn, ziache kwa dakika 10. Kisha epua acha zipoe.
- Weka kwenye brenda, ongeza maziwa kisha saga. Muekee mtoto ajirambe.
- Kikibaki hifadhi kwenye jokofu (freezer), kinaweza kutumika wiki 4 usizidishe