JINSI YA KUTENGENEZA KARANGA ZA MAYAI
Mahitaji:
-Karanga kilo moja.
-Mayai 2-3 inategemea na ukubwa.
-Chumvi kijiko kimoja.
-Sukari kiasi unachohitaji.
-Unga wa ngano robo kilo(kidogo tu).
-Mafuta ya kupikia.
Kuandaa:
-Chukua karanga weka katika sinia, chambua kuondoa karanga mbovu,zilikatika na taka taka.
-Baada ya kuchambua weka katika bakuli au chombo cha kukandia, piga mayai katika chombo pembeni na uweke -Chumvi. Tia mayai katika karanga na kisha zichanganye kuhakikisha zote zimekolea mayai.
-Chukua kiasi cha sukari unachokadiria kitakufaa Tia katika ule mchanganyiko wa karanga,mayai na chumvi kisha -Changanya ili sukari inate katika karanga zote.
-Chukua unga Tia Katika mchanganyiko wako, changanya vizuri kuhakikisha karanga zote zimekuwa nyeupe kwaku funikwa na unga

-Weka mafuta kiasi kwenye kikaango, yakichemka anza kukaanga karanga zako hakikisha unazitoa kabla hazijawa Brown sana usijeunguza karanga zako
ANGALIA VIDEO HII