JINSI YA KUPIKA KASHATA
VIPIMO
👉 Karanga - ½kg
👉 Sukari ya Brown - ½kg
👉 Maji - ¼ Cup
👉 Siagi - 1 KiJiko
NAMNA YA KUPIKA
1. Pasha sufuria jikoni kwa moto wa wastani. Zikaange karanga kwa dakika 4 - 5 kaanga hadi ziive, kuwa makini zisiungue kuwa nyeusi.
2. Zikiiva zitoe jikoni wacha zipoe toa maganda ili ziwe nyeupe.
3. Tumia moto mdogo na weka sufuria jikoni tia sukari na maji. Koroga taratibu hadi sukari na maji kuchanganyika na kunata huchukua kama dakika 6-7.
4. Mimina karanga kwenye mchanganyiko wa maji na sukari, changanya vizuri kwa dakika chache na zima jiko.
5. Pakaza sahani siagi na mimina mchanganyiko. Kisha tandaza vizuri wacha ipoe kwa dakika muda kidogo.
6. Kisha kata vipande ikiwa ya moto moto. Weka sehemu ya ubaridi ili kuganda. Baada ya hapo Kashata za karanga zitakuwa tayari kuliwa.
NB ; NI BIASHARA NZURI SANA ENDAPO UKIWEKA ENEO LENYE WAPITA NJIA WENGI AU WANAFUNZI 💚