JINSI YA KUANDAA JUISI YA EMBE NA NDIMU AU LIMAO.
MAHITAJI
Tikiti la asali (honey melon) - 1
Embe - 3
Tangawizi - 1 Kijiko
Ndimu - 1
Sukari - ¼ Kikombe cha chai
Arki rose - 2 Matone
Namna Ya Kutayarisha
- Limenye melon na ulikate kate kisha tia kwenye blender.
- Tia embe iliyokatwa katwa katika blender
- Kisha tia ndimu iliyokatwa vipande kiasi pamoja na maganda yake
- Halafu weka sukari
- Saga vizuri hadi ilainike
- Mimina kwenye jagi kisha tia matone mawili ya arki rose ukoroge na tayari kwa kunywewa
Kidokezo:
Ukiweka ndimu weka na maganda yake unapata ladha nzuri zaidi.