Vipimo
Ndizi mbivu zilizowiva sana - 4
Mafuta ya kukaangia - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Kataka ndizi kila moja kiasi ya vipande vitatu.
- Menya maganda, kisha kata kila vipande kwa urefu vitoke kiasi vipande vitatu kutegemea na ndizi yenyewe. Ikiwa ni nyembamba, kata mara mbili tu.
- Weka mafuta kiasi kidogo tu katika kikaango (frying pan) kisha kaanga ndizi.
- Zinapowiva upande mmoja geuza upande wa pili kaanga kisha zitoe uweke katika sahani zikiwa tayari.