Chukua bakuli safi, kwenye bakuli kamua malimao kisha toa mbegu zote, yabaki maji ya limao.
Washa jiko, bandika sufuria weka vikombe 2 vya maji, asali na tangawizi. Acha mchanganyiko uchemke kwa moto mdogo kwa muda wa dakika 10, mpaka asali iyeyuke na harufu nzuri ya tangawizi isikike.
Epua, acha ipoe. Chukua jagi safi. Kwenye jagi, weka maji ua limao, maji ya baridi vikombe 14 kisha weka mchanganyiko ulioutoa jikoni. Changanyanya vizuri weka kwenye jokofu kwa muda wa lisaa limoja. Kama utapenda weka majani ya mnanaa na giligilani ili kupata harufu nzuri.