Bandika sufuria jikoni, weka mafuta. Acha mafuta yapate moto kisha weka tambi, sukari, chumvi na iliki kwa pamoja. Kaanga kwa muda wa dakika 5 kwa moto mdogo ili kuzuia chakula kisiungue.
Weka maziwa yote huku ukiwa umepunguza moto kuepuka maziwa yasichemke na kumwagika. Acha tambi zichemke kwa muda wa dakika 7 kisha ongeza maji na koroga tambi. Endelea kukoroga mara kwa mara mpaka uone tambi zimeiva.