JINSI YA KUPIKA SAMBUSA ZA NYAMA

MAHITAJI
  • Nyama steki kilo 1 ( mi nina mashine ya kusagia kama huna nunua ya kusaga)
  • Vitunguu maji 2
  • Majani ya Giligiliani vifungu 2 
  • Garam masala kijiko 1 cha chai
  • Chumvi kijiko 1 cha chai
  • Pilipili manga kikijo 1 cha chakula
  • Kitunguu saumu kilichosagwa kijiko 1 cha chai
  • Tangawizi ya Unga kijiko 1 cha chai
  • Karoti 2 kubwa
  • Pilipili hoho 2
  • Unga wa ngano vijiko 4 vya chakula au ute wa yai
  • Manda
  • Butter kijiko kimoja cha chakula
JINSI YA KUANDAA
  • Bandika nyama weka chumvi, mpaka iive iwe laini. Hamisha supu pembeni ibaki nyama tu.
  • Chukua mashine ya kusagia nyama, weka giligilia kwenye nyama, anza kusaga nyama na giligiliani pamoja, funika weka pembeni.
  • Kata kata vitunguu maji, muundo wa box size ndogo sana, kata karoti na pilipili hoho. Weka pembeni.
  • Chukua frying pan pana, weka butter. Ikianza kuchemka weka vitunguu maji, karoti na pilipili hoho, koroga visiive.
  • Weka kitunguu saumu kilichosagwa, weka pilipili manga na tangawizi koroga vizuri.
  • Weka nyama, koroga vizuri ili ichanganyikane na viungo vingine, weka garam masala koroga dakika 2, epua. Usiifunike
  • Koroga unga wa ngano au ute wa yai, hii itakusaidia kufungia sambusa.
  • Chukua manda, kata kwa umbo la pembetatu. Kisha weka nyama kiasi, anza kufunga ila ukifika mwisho paka ute wa yai au unga wa ngano uliokoroga.
  • Inasaidia sambusa zisifunguke wakati wa kupika.
  • Bandika mafuta yakipata moto anza kupika,mpaka uone sambusa zimegeuka rangi na kua kahawia

ANGALIA VIDEO HII

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad