Mahitaji
Maelekezo
- Chemsha mafuta mpaka yachemke, weka unga kwenye bakuli au sufulia.
- Weka chumvi, amira changanya. Chota mafuta vikombe viwili vya kahawa weka kwenye unga.
- Changanya vizuri na mwiko ( tumia mwiko sababu mafuta ni ya moto). Endelea kuchanganya na mikono mpaka unga uwe mlaini kabisa.
- Uchanganyikane na mafuta vizuri, chukua tui weka sukari na vanila. Tui liwe la uvuguvugu, koroga mpaka sukari iyeyuke.
- Weka kwenye unga, endelea kukanda. Kanda mpaka uone ukinyanyua unga kwa vidole, unanyanyuka wote haubaki kwenye sufuria.
- Mwagia mafuta ya uvuguvugu juu ya unga uliokanda huku ukiendelea kukanda mpaka mafuta yasionekane kwenye unga.
- Funika kwa dakika 5 uumuke,kisha anza kusukuma na kukata.Kata staili unayopenda.
- Bandika mafuta jikoni. Yakipata moto weka maandazi yakigeuka rangi na kua kahawia geuza upande wa pili.
- Ukiona yameiva epua. Tayari kwa kujiramba.