KUANDAA WALI WA BIRIANI

WALI WA BIRIANI
  • Mchele kilo 1
  • Nyama kilo 1
  • Samli ½ kilo 
  • Mbatata ½ kilo 
  • Vitunguu maji kilo 1
  • Thomu gram 150
  • Tangawizi mbichi gram 150
  • Hiliki gram 50
  • Mdalasini gram 100
  • Mtindi painti 1
  • Siki kiasi
  • Majani ya nanaa fungu moja
  • Chumvi kiasi
  • Zaafarani kidogo (irowekwe kwa maji ya moto nusu kikombe cha kahawa)
  • Tungule ilosagwa
  • Tungule ya kopo
JINSI YA KUANDAA

  1.          Menya vitunguu maji uvioshe uvikate. teleka sufuria utie samli, ikichemka tia vitunguu uvikaange bila ya kuvivuruga mpaka viwe vyekundu. Vichuje uvitoe halafu vitandaze katika sinia.
  2.         Twanga mdalasini na hiliki mpaka viwe laini kama unga. Menya thomu uitwange pamoja na tangawizi mbichi.
  3.         Kata nyama vipande vikubwa kisha tia chumvi na vitu ulivyovisaga (yaani tangawizi mbichi na thomu) vile vile tia unga unga wa mdalasini na hiliki pamoja na mtindi wa maji. Pika mpaka karibu nyama kuiva kabisa ndipo utie mbatata. Ukiona mbatata zimeshaiva tia siki.Usiache kukauka kabisa, bakiza rojorojo. Tia maji katika sufuria na chumvi yakichemka tia mchele. Acha utokote, angalia kiini cha wali ukiona umeshaiva uchuje.
  4.        Angalia sufuria ya nyama na rojo lake lisiwe limekauka kabisa, lazima ziwe na maji kidogo. Chukua vile vitunguu ulivyovikaanga vikapoa uvinyunyuzie juu ya masalo yote (usikoroge). Halafu utie mchele uliouchuja, nyunyuzia maji ya zaafarani juu ya wali wote halafu unyunyuzie samli ile uliyochuja kutoka kwenye vitunguu ulivyovikaanga ienee juu ya wali wote. Kisha funika upalie makaa.
  5.             Wali ukishakuwa tayari utaupakua. lakini unapotaka kuupakua lazima kwanza uutoe wali wote mweupe uutie katika chombo chengine, halafu uyakoroge masalo yachanganyike sawasawa kisha ndio uyatie juu ya wali katika kila sahani.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad