JINSI YA KUPIKA MKATE WA NYAMA

MALIGHAFI
Vipimo
  1. Nyama ya kusaga -  ½ LB
  2. Kitunguu maji kilichokatwa kidogo - 1
  3. kidogo (chopped)
  4. Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi iliyosagawa - 1 Kijiko cha chai                   
  5. Pilipili manga ya unga - 1 kijiko cha chai
  6. Unga wa ngano-  2-3 vikombe
  7. Hamira - 1  au  1½ kijiko cha chakula 
  8. Chumvi -  ½ kijiko cha chai
  9. Mayai -  5
  10. Siagi -  225g


Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
  1. Tia katika nyama thomu, tangawizi, chumvi, pilipili manga, (ukipenda bizari zako nyingine), vitunguu, kisha iache kama muda wa saa moja ili vikolee hivyo vitu kwenye nyama.
  2. Ikaushe nyama  mpaka iwive kama nyama ya sambusa.
  3. Vunja mayai manne na la tano liache pembeni. Yatie kwenye bakuli upige kama kiasi cha dakika mbili.
  4. Tia unga kwenye mayai na changanya vizuri kisha tia hamira na chumvi halafu changanya kwa sekunde chache tu.
  5. Halafu tia siagi kwenye bakuli la unga na uchanganye vizuri mpaka uchanganyike vizuri yaani lifanyike donge halafu uzunguushie karatasi ya plastiki (plastic wrap) au mfuko wa plastiki, na uweke kwenye friji kwa usiku mzima ulale yaani ni vizuri ulale siku nzima ili ladha yake itokeze.
  6. Siku ya pili toa unga kutoka kwenye friji na uweke kwa muda wa saa moja ili ukande kwa kutumia siagi na lile yai moja lililobakia mpaka uwe laini.
  7. Sukuma kwa kifimbo kama unataka kufanya chapati, yaani utandaze kwa kifimbo halafu ukishakua bapa (flat) chukua nyama yako itandaze juu ya ule mkate yaani nyunyiza kwenye ule unga ulioutandaza.
  8. Kunja unga (roll)  na nyama yake ukisha unauzunguusha duara ili kuutia kwenye treya yako ya kubake unauacha uumuke.
  9. Ukishakuumuka unapaka siagi au yai juu yake ukisha unaupika katika jiko (oven) kama unavyopika mikate mengine kwa moto wa 350 Deg. Na kwa muda wa kama dakika 20 au zaidi hadi uwive.
Ni vizuri kuliwa kwa  chai au juice

ANGALIA VIDEO HII

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad