MAHITAJI NA MALIGHAFI
1. Sulphonic(LABSA) 2. Slec 3. Pafyumu (lemon)
4. Rangi (kijani/ nyekundu/ blue)
5. Chumvi nzuri ya mawe.
6. Glycerin
7. Soda ash light.
8. Formalin na alka.
9. Maji yaliyokuwa safi .
10. Chombo zaidi ya lita 25.
JINSI YA KUTENGENEZA
1. Chukua sulphonic 1 lita moja weka katika chombo chako cha kutengenezea(lita 25) .
Kisha chukua slec yako weka katika kile chombo ambacho uliweka sulphonic kisha changanya kwa pamoja.
Chukua soda ash nusu kilo kisha iloweke katika maji lita 5 katika chombo kingine pembeni , kisha chukua mchanganyiko wako huo na mimina katika chombo chako chenye mchanganyiko wa sulphonic na sles weka maji lita 15 koroga kwa dakika 10 kuwa makini kwasababu utavimba sana.
Kisha weka vijiko vya chai 2 mpaka 3 vya rangi kutokana na rangi unayoitaka lakini angalia isizidi sana koroga tena vizuri.
Kisha chukua glycerin vijiko 2 vya chai kisha weka katika mchanganyiko wako wa sabuni katika chombo chako na mpaka hapo sabuni itaanza kuonekana .
. Kisha weka 25ml yani kwa kiasi unachotaka pafyumu (lemon) , hii itafanya sabuni yako inukie kwa harufu vizuri.
Koroga chumvi ya mawe pembeni kiasi kidogo tu kama vijiko 6 ya chai kisha mimina katika mchanganyiko wako na malizia kiasi cha maji mpaka kufikia lita 25 ambazo ni wastani kabisa.
NB , Chumvi ikizidi itafanya sabuni yako kuwa inachelewa kutoa povu kwahiyo kuwa makini sana.
Kisha weka alka nusu changanya vizuri na mwisho malizia kwa kuwekaformalin kisha koroga tena vizuri. (alka na formalin sio lazima sana hata kama hautavitumia sabuni yako itakamilika na itakuwa poa kwa matumizi ).
ANGALIZO
1. Mchanganyiko wako utatoa sabuni lita 25 zikizidi hapo zitakuwa sio nzito kwahiyo kuwa makini.
2. Kuna baadhi ya malighafi ni sumu kwahiyo tumia vifaa vya kujikinga kama MASKI NA GLOVES
ANGALIA VIDEO HII